
Dira (Vision)
Kuwawezesha wakulima kupata mafanikio ya juu katika kilimo endelevu kupitia teknolojia ya kisasa na maarifa bora ya soko.
Dhamira (Mission)
Kutoa huduma za hali ya juu za bima ya mazao, ufuatiliaji wa mazao, kugundua magonjwa, ufikiaji wa masoko na bei kwa wakulima, ili kuboresha usimamizi wa mazao, kuongeza mavuno, na upataji faida kwa uwazi na ufanisi.

Misingi ya huduma zetu (Core Values):
- Ubunifu: Kukuza na kutumia teknolojia ya kisasa kwa ufanisi katika kilimo.
- Uendelevu: Kuunga mkono mbinu za kilimo ambazo zinahakikisha uzalishaji endelevu na utunzaji wa mazingira.
- Uwazi: Kutoa taarifa sahihi na wazi kwa wakulima kuhusu bima ya mazao, hali ya mazao na masoko.
- Ushirikiano: Kujenga ushirikiano wa moja kwa moja kati ya wakulima, maafisa ugani na wanunuzi wa mazao ya kilimo kwa manufaa ya pande zote.
- Ufanisi: Kuongeza faida kwa wakulima kwa kupunguza upotevu na kuongeza mavuno kupitia hatua za haraka na sahihi.
- Uadilifu: Kufanya kazi kwa uaminifu na uwajibikaji katika kutoa huduma zetu kwa wakulima.